Kocha mkuu wa Bayern Munich Julian Nagelsmann amekiri kwamba hajui kwanini Leroy Sane hachezi kwa kiwango bora kwa Bayern Munich kwa sasa.

Sane ambaye alihamia Bayern Munich akitokea klabu ya Manchester City alifikisha mchezo wa 40 dhidi ya Augsburg msimu huu siku ya Jumamosi lakini alitolewa dakika ya 65 na nafasi yake ilichukuliwa na Kingsley Coman baada ya kushindwa kucheza vizuri.

Sasa bosi huyo wa Bayernn anahisi winga huyo wa miaka 26 anapitia kipindi cha kigumu ambacho kimekuwa kawaida katika maisha yake ya soka hadi sasa, lakini bado ana imani na uwezo wake.

“Nampenda Leroy sana, kama mtu na kama mchezaji. Kila mtu anajua kwamba ana sifa za ajabu,” Nagelsmann aliambia GOAL na SPOX.

“Anajikosoa vya kutosha na anajijua kuwa hajacheza vizuri hivi karibuni. Sijui kwanini haswa.

“Amekuwa na misukosuko katika maisha yake. Ninamuunga mkono kabisa.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa