Nigeria Watinga 16 Bora Michuano ya AFCON

Nigeria imepata nafasi ya kufuzu katika hatua inayofuata ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika inayoendelea nchini Cameroon. Super Eagles waliilaza Sudan 3-1 Jumamosi na sasa wanaongoza Kundi D.

Nigeria Watinga 16 Bora  Michuano ya AFCON

Beki wa Nigeria William Troost-Ekong alisisitiza dhamira yake ya kushinda mashindano hayo kwa mwaka huu 2022.

“Leo ilikuwa changamoto tofauti. Nafikiri mchezo wa kwanza kila mmoja aliona tunachoweza kucheza. Kipindi cha kwanza, nilifikiri tulikuwa polepole, lakini kipindi cha pili tulitoka vizuri. Lakini bado ni dalili nzuri kuona. Hata pale ambapo hatujafanya vizuri kama mchezo wa kwanza.Katika baadhi ya vipengele bado tunafanikiwa kufunga mabao.Na nadhani bado tunastahili kushinda mchezo huu.Yote kwa yote,furaha sana.Pointi sita… Muhimu. Na hadi raundi inayofuata, lakini kwa hakika, tunataka kushinda mchezo wa mwisho pia”. 

Pia katika Kundi D, Misri iliifunga Guinea-Bissau 1-0 baada ya kushindwa na Nigeria kwenye mechi ya ufunguzi ya Kundi hilo.

Siku ya Jumatano, Misri itamenyana na Sudan na Guinea-Bissau itacheza dhidi ya Nigeria.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe