Nyota wa Real Madrid Karim Benzema atarejea Ligue 1 Lyon, hii ni kwa mujibu wa wakala wake Karim Djaziri.

Benzema alipitia katika akademi ya Lyon na alikaa miaka mitano na timu ya wakubwa hadi alipojiunga na Madrid mwaka 2009, baada ya kujiimarisha kama mmoja wa wachezaji wachanga wa Ulaya anayeahidi kufuatia kushinda mataji manne mfululizo ya Ligue 1.

Nyota wa Madrid Benzema Kurejea Lyon - Djaziri.

Tangu ahamie Madrid, Benzema ameshinda mataji manne ya Ligi ya Mabingwa na mataji matatu ya LaLiga.

Lakini Djaziri alidokeza juu ya kurudi kwenye klabu ya utotoni ya Lyon kwa mshambuliaji huyo wa miaka 33.

“Je! Karim Benzema atarudi Lyon? Ndio, kwa kweli nadhani atarudi,” Djaziri aliiambia Inside Gones.

“Anazungumza nami kila wakati na anaangalia mechi zote za timu.

“Juu ya hayo, hajawahi kwenda kwenye Uwanja wa Groupama na akilini mwake ni kitu anachotaka, ana Lyon moyoni mwake.”

Benzema amefunga mabao 10 ya LaLiga kwa mabingwa watetezi Madrid msimu huu baada ya ushindi wake wa mabao 4-1 dhidi ya Deportivo Alaves Jumamosi.

Kwa jumla, Benzema amepachika mabao 15 kwenye mashindano yote msimu 2020-21.

Benzema amefunga angalau magoli 15 katika misimu 10 kati ya misimu 11 aliyoichezea Madrid katika mashindano yote.


MSHINDANI HUSHINDA BWANA!

Anayejaribu hawezi kutoka kapa Meridianbet! Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet inakuhakikishia ushindi mkubwa kila unapojaribu kuingia mchezoni. Washindi hushindana, ingia mchezoni!

Fairy-in-Wonderland_Casino-Post_25-January

CHEZA SASA

12 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa