Pacha wa Messi Kulikosa Kombe la Dunia

Giovani Lo Celso anaripotiwa kukabiliwa na kinyang’anyiro dhidi ya muda kuwa fiti kwa Kombe la Dunia baada ya kuumia wikendi iliyoisha.

Kiungo huyo wa kati wa Argentina alilazimika kutolewa nje baada ya dakika 25 pekee, wakati Villarreal ilipopokea kichapo cha 1-0 ugenini dhidi ya Athletic Bilbao Jumapili.

 

kombe

AS Sport sasa wameripoti kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, ambaye yuko kwa mkopo kutoka Tottenham ni shaka kubwa kwa Kombe la Dunia kutokana na jeraha la misuli ya paja.

Villarreal wanatarajiwa kufanya majaribio zaidi siku zijazo ambayo yatabainisha iwapo atakuwa fiti kwa wakati kwa ajili ya kuanza kwa michuano hiyo.

Argentina wataanza kampeni yao dhidi ya Saudi Arabia mnamo Novemba 22 huko Lusail.
Lo Celso ni mchezaji muhimu wa Argentina, na walianza tisa katika michezo kumi na moja, katika mechi 17 za kufuzu Kombe la Dunia.

 

kombe

Atakuwa na nia ya kudhihirisha utimamu wake kabla ya mchuano huo, huku Argentina ikiwa ni miongoni mwa wanaopewa nafasi kubwa ya kushinda kombe hilo nchini Qatar.

Lo Celso yuko katika msimu wake wa pili kwa mkopo katika klabu ya Villarreal baada ya kuhangaika kufanya makubwa Tottenham. Awali alijiunga na klabu hiyo Januari mwaka huu, kabla ya mkopo wake kuongezwa kwa msimu huu.

Tangu aanze kucheza mechi ya kimataifa mwaka 2017 katika mechi ya kirafiki dhidi ya Urusi, ameichezea nchi yake mara 41 ambapo amefunga mabao mawili. Pia alikuwa sehemu ya kikosi kilichoshinda Copa America, kikianza katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Brazil kwenye fainali.

Acha ujumbe