Gerard Pique ambaye ni beki wa kati wa timu ya Barcelona amekiri kwamba anatumaini klabu inaweza kumsajili starika Erling Haaland wa Borussia Dortmund wakati huu wa majira ya joto.

Pique: Haaland Anaweza Kutua Camp Nou

Uchumi wa Blaugrana upo katika hatari, lakini bado kuna matumaini kwamba wangeweza kumleta mchezaji mwenye jina kubwa Camp Nou msimu huu wa joto.

“Sijui, natumai kwamba atakuja Barcelona,” Pique alisema wakati wa mazungumzo na YouTuber Ibai Llanos.

“Wachezaji wazuri wanapaswa kuwa nasi, lakini huo ni uamuzi kwa klabu kufanya. Watajua.”

Sergio Aguero mwenye umri wa miaka 33 amejiunga na Barcelona bila malipo na Pique amekiri kwamba wana uhusiano wa awali.

“Tayari nilikuwa na uhusiano mzuri naye. Kwa miaka, tumekuwa tukiunganishwa kwenye media ya kijamii,” alisema.

“Nilicheza Kombe la Dunia la U20 dhidi yake, kwa sababu sisi ni wa kizazi kimoja. Leo Messi anamzungumzia vizuri sana.”

Kulikuwa na mazungumzo wakati wa kiangazi kilichopita kwamba Barcelona ingejaribu kuhamuuza mchezaji huyo wa miaka 34, lakini hakusudii kucheza klabu nyingine.

“Siku nitakapoacha kucheza Barcelona nitaacha mpira, sitaenda kwenye timu nyingine,” Pique alisema.

“Ikiwa hawanitaki, kama Ronald Koeman ataniambia niondoke, basi ndio hivyo. Nina shauku tu ya kucheza Barcelona. Singekuwa na motisha ya kuvaa jezi nyingine.”


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa