Kocha mkuu wa Juventus Andrea Pirlo amesema kwamba Wachezaji wa Juventus bado wanaamini kuwa wanaweza kutwaa taji la 10 mfululizo la Serie A msimu huu.

Bianconeri wako nyuma kwa vinara Inter kwa alama 10, ingawa wana mchezo mkononi kwa upande wa Antonio Conte.

Amesema hayo kuelekea mchezo dhid ya Spezia siku ya Jumanne, na Juve wanatafuta alama tatu muhimu baada ya kutoshinda katika katika michezo yao mitano iliyopita kwenye mashindano yote.

Licha ya pengo la Inter, Conte anasisitiza kuwa kikosi chake hakijakata tamaa ya kunyakua Scudetto nyingine.

“Sitasema tunaweza tunaikimbizia Scudetto kama sikuwa najua kwamba timu inafikiria hivyo pia,” aliambia mkutano wa waandishi wa habari Jumatatu.

“Najua vijana hawa wanaamini, wanafanya mazoezi vizuri na wanataka kurudi kushinda taji na hii inanifanya nijisikie raha.

“Hatuangalii ni nani aliye juu yetu au nyuma yetu, tunakaza sisi wenyewe. Lengo lazima libaki vile vile. Kuna michezo mingi bado, tutakuwepo.

“Lengo la awali lilikuwa kuwashinda wote, tunajua tulipoteza alama chache, lakini hiyo ni ya zamani. Lazima tuangalie mchezo ujao ni Spezia.”

Juve imeshinda mara 21 kati ya mechi 23 za nyumbani za Serie A dhidi ya timu zilizopanda daraja, ikiweka cleen sheet 14 katika mechi hizo zote.


Ni Muda wa Kuvuna Mkwanja na Jungle Jim and the Lost Sphinx

Hauihitaji kufikira mara mbili ni mchezo gani utakupatia mkwanja ndani ya kasino za Meridianbet. Jiunge sasa ufurahie Jungle Jim and the Lost Sphinx.

Juventus, Pirlo: Juventus Haijakata Tamaa Kushinda Serie A, Meridianbet

  CHEZA HAPA

9 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa