Nahodha wa Real Madrid Sergio Ramos ameachwa kwenye kikosi cha mwisho cha Uhispania kwaajili ya Euro 2020, lakini Aymeric Laporte wa Manchester City amejumuishwa baada ya kubadili urai wa Ufaransa.
Bosi wa Uhispania Luis Enrique alitaja jopo lake la vijana 24 kwa mashindano haya ya kiangazi mwezi Mei 24, na Ramos akikosa baada ya msimu mgumu wa kukatisha tamaa huko Real.
Sergio Busquets wa Barcelona ameteuliwa kuwa nahodha wakati Ramos hayupo, wakati Laporte amepewa nafasi ya ulinzi mbele ya mchezaji huyo wa miaka 35 baada ya kuona ombi lake la kuiwakilisha La Roja badala ya Ufaransa kupitishwa mapema mwezi huu.
Enrique alielezea maamuzi yake kumuondoa Ramos katika malenngo yake baada ya kukitangaza kikosi chake, aliwaambia maripota: “Ramos hakuwa na uwezo wa kiushindani msimu huu, hakuweza kufanya mazoezi na wenzake. Nilimpigia jana usiku ilikuwa ngumu na ni ngumu”
“Nalazimika kusema kwamba ni maamuzi magumu,Nilipendekeza atakuwa mbinafsi na kwamba arejeshe kiwango chake cha kucheza katika klabu yake na katika timu ya taifa.”
Kikosi Kamili cha Spain cha Euro 2020:
Magolikipa:Â David de Gea, Robert Sanchez, Unai Simon
Walinzi:Â Aymeric Laporte, Jose Gaya, Jordi Alba, Pau Torres, Eric Garcia, Diego Llorente, Cesar Azpilicueta
Viungo:Â Marcos Llorente, Sergio Busquets, Rodri, Pedri, Thiago, Koke, Fabian
Washambuliaji:Â Dani Olmo, Mikel Oyarzabal, Gerard Moreno, Alvaro Morata, Ferran Torres, Adama Traore, Pablo Sarabia
BONASI YA 50% KILA SIKU KATIKA KASINO ZA EVOPLAY HAPA MERIDIANBET.
Meridianbet na Evoplay Kasino wanakupa bonasi ya 50% ya kiasi utakachoweka katika akaunti yako leo. Unasubiri nini ni wakati wa kupiga pesa sasa na Mabingwa.
Asikate tamaa wakati bado upo