Rangers Wamtolea Macho Ronald Koeman

Baada ya Steven Gerrard kuwapa mkono wa kwa heri sasa Rangers wanatafuta kocha mbadala ili kuendeleza wimbo mzuri ambao Gerrard aliuanzisha na Ronald Koeman anaonekana kuwa mtu sahihi Ibrox Stadium kwa Mabingwa wa Scottish Premiership.

Gerrard aliondoka rasmi Rangers siku ya Alhamisi baada ya kufikia makubaliano na klabu ya Aston Villa ya kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo kufuatia kumfuta kazi Dean Smithwikendi iliyopita sababu ya kiwango duni kuanza kwa msimu huu.

Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani ni kwamba mabingwa hao watetezi wa Scottish Premiership wanamtazama Ronald Koeman kama mbadala sahihi, Koeman alitimuliwa na Barcelona mnamo Oktoba 28.

Rangers wanaongoza ligi kwa sasa na mwaka uliyopita walimaliza utawala wa Celtic wa kutwaa taji hilo mara tisa mfululizo, wakati huohuo mwandishi Fabrizio Romano ni kwamba mchezaji wa zamani Rangers na kocha wa Feyenoord Giovanni van Bronckhorst kwa sasa ndiye kocha ndiye kocha anayepewa nafasi ya kuchukua mikoba ya Gerrard.


NJIA RAHISI YA MKWANJA NA TITAN DICE

Unawezaje kuikosa hii! njia rahisi ya kutengeneza mkwanja katika kasino maridhawa za meridianbet. Muda wa kufurahia na kutengeneza mkwanja ipo mikononi mwako unasubiri nini?

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA SASA

Acha ujumbe