Mchezaji wa zamani wa Manchester City na Real Madrid, Robson de Souza maarufu kwa jina la Robinho, amehukumiwa kifungo cha miaka tisa jela kwa makosa ya unyanyasaji wa kijinsia na ubakaji.
Mahakama nchini Brazil iliamua kwamba mchezaji huyo wa miaka 40 atatumikia kifungo chake katika nchi yake licha ya kosa hilo kufanyika nchini Italia mwaka 2013.
Robinho alipatikana na hatia kwenye mahakama ya Italia mwaka 2017 kwa kushiriki ukatili huo kwa mwanamke Malbanyani mwenye umri wa miaka 22. Beti na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara.
Mshambuliaji wa zamani amekuwa akiishi Brazil na ataendelea kuwa huru wakati akisubiri rufaa dhidi ya hukumu hiyo. Odds kubwa, kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni njia rahisi ya kukupa mtonyo mrefu. Ingia mchezoni hapa.
Robinho alikuwa akicheza kwenye klabu ya Serie A AC Milan wakati wa kosa hilo baada ya kujiunga na klabu hiyo kutoka Manchester City mwaka 2010.
Nyota huyo alipatikana na hatia baada ya kupoteza rufaa mwaka 2020 kabla ya mahakama kuu ya Italia kuthibitisha hukumu yake mwaka 2022.
Waranti wa kimataifa wa kukamatwa ulitolewa baadaye na mawakili wa Italia.
Robinho bado anasisitiza kwamba kitendo hicho kilikuwa ‘kwa makubaliano’ baina ya pande zote mbili.
Robinho alitambulishwa kama usajili wa kwanza wa kutisha wa Manchester City katika enzi yao mpya alipoizamisha Real Madrid kwenye dimba la Etihad Stadium mwaka 2008 kwa usajili wa pauni milioni 32.5.
Usajili wake ulifanyika siku ya mwisho ya uhamisho na siku ya kwanza ya utawala wa Sheikh Mansour kama mmiliki wa Manchester City.
Baadaye alihama kwenda AC Milan, ambapo alidumu kwa miaka mitano iliyofuata kabla ya kujaribu bahati yake nchini China na klabu ya Guangzhou Evergrande.
Amewahi kukipiga pia kwenye vilabu vya Atletico Mineiro ya Brazil na klabu ya Uturuki ya Sivasspor na Istanbul Basaksehir kabla ya kutundika daruga mwaka 2020 na Santos. Jisajili na Meridianbet upate bonasi za kasino kibao na odds kubwa za ubashiri kwa machaguo kibao.