Cristiano Ronaldo ameonyesha kuwa hana mpango wa kustaafu kwa kusema anatarajia kucheza kwa “miaka mingi” licha ya kujiandaa kutimiza miaka 36 mwezi Februari.
Fowadi huyo wa Juventus hajaonyesha dalili zozote za kupunguza kasi ya ubora wake,baada ya kumaliza msimu wa 2019-20 akiwa na mabao 31 na taji la pili la Serie A.
Mwaka 2020 alikua mchezaji wa nne kwenye historia ligi ya Italia kwa kufunga mabao 33 baada ya kufanya hivyo Omar Sivori (33 mwaka 1961), Gunnar Nordahl (36 mwaka 1950) na Felice Borel (41 mwaka 1933).
Idadi hiyo inamuweka juu ya chati ya ufungaji katika ligi tano bora za Ulaya mwaka huu, mbele ya mshindi wa tuzo ya Mchezaji Bora wa Wanaume FIFA Robert Lewandowski (32).
Nahodha wa Ureno Ronaldo atakuwa na umri wa miaka 37 wakati Kombe la Dunia la 2022 linatarajiwa kuanza kurindima nchini Qatar lakini alidokeza kuwa anatarajia kuwapo.
“Haijalishi umri. Kilicho muhimu ni akili,” Ronaldo aliiambia BBC Sport, baada ya kuteuliwa kuwa Mchezaji wa Karne katika Tuzo za Soka za Globe wiki hii.
Ronaldo alifunga bao katika ushindi wa 3-0 wa Juventus dhidi ya Barcelona kwenye Ligi ya Mabingwa mnamo Desemba 8.
Licha ya kuwa katika fomu ya kuvutia, Bianconeri wako nafasi ya sita kwenye jedwali, alama 10 nyuma ya vinara wa ligi Milan, na Ronaldo alikiri kukosekana kwa mashabiki kwenye Uwanja wa Allianz kulimkatisha tamaa.
“Sipendi kucheza kwenye viwanja bila mashabiki, ni kama kuruka sarakasi lakini hauoni vichekesho,” Ronaldo alisema.
VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!
Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini?
Adelta
Ronald Bado yuko vizuri
Neema juma
Yuko sahihi Ronaldo
Tatu
Ronaldo anajua mpira
Sabrina
CR7 yupo vizuri
Fatina mfingi
Ronald yuko vizur
Ernest Kimeru
Bado yupo vizuri cha msingi majereha yampitie pembeni tuu
Caroline
Ni vizuri kwa sababu bado tunamuhitaji
warda
Bado yuko fiti
Dorophina
Ronaldo bado yupo fiti anamuda mwingi wa kucheza
Angelina
Cr7 bado ananguvu acha apambane
Rahmal
Ronaldo Yuko poa sana
Janeflora malisa
Safi sana
Sarah
Yuko vizuri Ronaldo
Hopemwaikuka
Anaweza mazoez yapo
Sania
Ronaldo bado anadai
Issa
Mzee wa rekod