Kocha wa muda wa Manchester United Ralf Rangnick amethibitisha mshambuliaji Christiano Ronaldo alirejea mazoezini na anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi kitakachomenyana na Tottenham leo katika uwanja wa Old Trafford.
Ronaldo alikosa mchezo wa kupoteza kwa 4-1 dhidi ya City ambao ni mahasimu wao wa jiji la Manchester na ilisemekana kwamba alikuwa akisumbuliwa na jeraha hali iliyopelekea kusafiri mpaka Ureno lakini taarifa kutoka vyanzo mbalimbali zilidai ni kutoelewana kwa nyota huyo na kocha.
“Alirejea tena mazoezi jana,” Rangnick alisema katika mkutano wake na waandishi wa habari kabla ya mechi siku ya Ijumaa.
“Alifanya mazoezi katika kipindi chote cha mazoezi na ninatarajia afanye mazoezi leo pia.
“Alifanya mazoezi vizuri, kama kundi lingine. Ningefikiri angepatikana kesho.”
Ronaldo amefanikiwa kufunga bao 1 pekee bila asisti kwenye michezo 10 msimu huu kwenye mashindano yote. Leo atamaliza ukame wake dhidi ya timu ya Conte?
Mchongo mpya mjini ni Shindano la Evoplay Spring Aweking katika kasino maridhawa za meridianbettz. Pata mgao wako wa TSh 25,000,000 katika michezo kibao ya kasino na sloti ziliyochaguliwa kushiriki.