Ligi kuu ya nchini Italia Serie A imetangaza sheria mpya kwamba vilabu vyote havitaruhisiwa kuvaa jezi za kijani.
Timu chache za ligi ya Italia zina tumia rangi ya kijani kibichi kwenye mavazi yao, kwa hivyo vilabu hivi vitaathiriwa vipi – na kwanini sheria hiyo imetekelezwa?
Serie A imepiga marufuku vifaa vya kijani vilivyovaliwa na wachezaji wa nje kwa madhumuni ya uwazi wa runinga.
Jezi za nyumbani, hata hivyo, zinaeleweka kuwa huru kutokana na sheria hii, na marufuku hii inatumika kwa jezi ya ugenini na ya tatu.
Iliripotiwa kuwa jezi za kijani zitapigwa marufuku kwa sababu ya rangi kufanana na nyasi kwenye uwanja, ambayo inaweza kuwachanganya watazamaji nyumbani.
Sheria hiyo itatumika tu kwa wachezaji, pamoja na soksi na kaptula, kwa hivyo walinda lango hawatoathiriwa chini ya sheria hii. Ikiwa jezi itajumuisha rangi tatu tofauti, kivuli kisicho kijani lazima kitumike kama rangi kuu.
Marufuku hii itaanza kuafanyakazi kuanzia msimu wa 2022-23 na kuendelea.
Serie A ilitangaza mabadiliko ya sheria mwaka huu mapema ili vilabu na watengenezaji wa jezi wawe na wakati unaofaa wa kubadilisha jezi zao ipasavyo.
SHOOT! mchezo unaokupa nafasi ya kupambania ushindi wako mkubwa kwenye kasino ya mtandaoni ya Meridianbet! Usisubiri hii, jiunge sasa kufurahia ushindi!
Angelina
Duuh hatari sana