Saleh Karabaka Vua Kinyago Wewe Ni Emmanuel Okwi

MAONI YA MWANDISHI WETU:

Baada ya kutangazwa kusajiliwa na Miamba ya Soka Tanzania klabu ya Simba SC, Kiungo mshambuliaji anayetokea ardhi ya Mama KIZIMKAZI, ardhi ya Hussein Mwinyi kwenye mizimu ya Mzee Karume. Anaitwa Saleh Kabaraka kinda mwenye miaka 23 tu lakini ana kipaji kikubwa alichojaliwa na mungu.

saleh karabaka
Kiungo Mpya wa Ushambuliaji wa Simba SC Saleh Karabaka akikabidhiwa pesa taslim baada ya kuonesha kiwango kizuri kwenye mchezo wa Kombe la Mapinduzi, uliomalizika kwa Simba kushinda 1-3, Bao la Tatu akifunga mwenyewe.

Wengi waliuponda usajili huo wakisema kwamba sio mchezaji mzuri, huku wengine wakisema kwamba anakwenda kuua kipaji chake lakini Master Benchika akawatuliza na kuwaambia tulieni ninyi niwaoneshe kilicho ndani ya huyu kijana. Odds kubwa kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni vitu vinavyoweza kubadilisha maisha yako kwa kukupatia pesa nyingi. Ingia mchezoni hapa.

Ni kipindi cha Pili Saleh Karabaka kwa sasa mitandaoni wanamuita KARABA, alinyenyuliwa na kupewa nafasi ya kuonesha uwezo wake dhidi ya waajiri wake wa zamani JKU, mpira wake wa kwanza anagusa anaaznisha shambulizi kwa kasi ya treni ya SGR anakimbia na kukaa kwenye nafasi nzuri ya kupokea mali kutoka kwa kinda mwenzake Mohamed Mussa, Touch yake a pili akapiga krosi kwenye tight and Impossible angle mpira uliomshinda kipa na kuusukumia wavumi.

Beti na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara Ligi kuu ya NBC.

Kijana wa watu anashindwa kushangilia goli lake la kwanza akiwa na Simba SC anaenda kupiga goti ishara ya kuomba msamaha, kisha naiona jezi namba 4 mgongoni ikimkumbatia kwa upendo mkubwa kijana yule, bila shaka ni Jean Othos Baleke na Fabrice Ngoma wanampongeza kijana, mara kwenye kundi hilo la wachezaji wengi wa Simba namuona nahodha kiongozi Shomari Kapombe- Shomy The Way akimpongeza kijana kwa kumpapasa kichwani na kumwambia karinu Msimbazi well done pambana.

” Kapteni (John Bocco) aliniambia sikia ukipata nafasi wewe cheza kama unavyocheza kawaida usiogope chochote” Saleh Karabaka (KARABA) akieleza namna ambavyo mchezaji mkongwe wa timu ya Simba na nahodha mkuu John Bocco alivyompa maneno ya kumuongezea kujiamini ndani ya uwanja.

“Kuna wachezaji wenzangu walinambia leo utafunga, kocha akikupa nafasi ya kucheza, alikuwa ni Ngoma na Baleke, walinambia utaifunga timu yako ya zamani. Lakini pia Kocha (Benchika0 alinambia ukiwa ndani cheza nyuma ya watu, kaa kwenye chaki (Mstari wa mwisho) nilifanya kama hivyo, nikapewa pesa kisha nikafunga” Saleh Karabaka.

Kijana huu ni ushauri tu utasemwa sana, utakosolewa sana na bado kuna watu watakusifia unapopatia, usivunjike moyo bado una safari ndefu Simba imekuamini nenda kaoneshe ulichojaliwa na Mungu, hakika una kipaji sina shaka na kiwango chako najua msimu uliopita ulikuwa na magoli 8 na asisti takribani 8, namba hazidanganyi, huenda ukawa CHAMA wa Unguja, wewe pia ni Vinicious Jr ajaye. Stand Up Man Pull Up Your Socks and Show us your gifted talents.

Odds kubwa, kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni vitu vinavyoweza kubadilisha maisha yako kwa kukupatia pesa nyingi. Ingia mchezoni hapa.

 

Acha ujumbe