Mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Bayern Munich Hasan Salihamidzic amesisitiza kwamba mshambuliaji Robert Lewandowski hatouzwa mwisho wa msimu huu na wataanza kufanya mazungumzo ya mktaba mpya hivi karibuni.

Salihamidzic: Tunaanza Mazungumzo na Lewandowski

Mkataba wa Lewandowski unatarajia kuisha mwishoni mwa msimu 2022-23 na iliripotiwa Bayern hataki kumuachia bure straika huyo hivyo wanaanza kuandaa mazingira ya kumbakisha.

Hivi majuzi Barcelona waliripotiwa kumtaka mshambulaji huyo na uvumi ulionyesha huenda Mpoland akatua Camp Nou baada ya rais wa Barca Joan Laporta kumjibu shabiki aliyemuuliza kama ni kweli Robert atasajiliwa na miamba hao wa LaLiga na Laporta alijibu “Lewandowski ana nafasi nzuri ya kusajiliwa.”

Salihamidzic alisema: “Tunataka kumbakisha Lewandowski tunamkubali sana, mashabiki wanampenda lakini pia ndiye mfungaji bora katika klabu. Tunaangalia uwezekano wetu wa kifedha na kiasi gani tunacho.

“nimeongea na Lewa na tutazumgumza na wakala wake. Anamkataba mpaka 2023. Hatuja zungumza bado lakini ndilo tutanataka kulifanya sasa.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa