Billy Joe Saunders atafanyiwa upasuaji katika uso wake baada ya kupigwa na Saul ‘Canelo’ Alvarez, hii ni kwa mujibu wa Promota Eddie Hearn.

Canelo aliongeza mkanda wa WBO katika kabati baada ya kumzibua Saunders katika raundi ya nane kwa TKO  huko Arlington, Texas siku ya Jumamosi.

Raia huyo wa Mexico alimpiga upper cut kali Saunders na pambano hilo lilikatishwa kabla ya kuanza kwa raundi ya tisa.

Saunders alipelekwa hospitalini mara tu baada ya pambano hilo na Hearn amethibitisha atahitaji upasuaji kwa mfululizo wa mapumziko karibu na tundu lake la macho.

Hearn alitwita hivi: “Tupo hospitalini Dallas, @bjsaunders_ alikaa usiku kucha. Alipata mateso mengi kwenye eneo la orbital na atafanyiwa upasuaji leo mchana.”

Akiongea baadaye, Canelo alisema alijua pambano hilo litasitishwa baada ya kumuharibu kwa kiasi mkubwa sura ya Saunders.

“Nilijua hii itakuwa matokeo ya mwisho,” Canelo aliiambia DAZN. “Niliijua. Nadhani nilivunja shavu lake na nilijua hatoki tena.

“Nilimwambia Eddie [Hearn] hatoki kwa sababu alivunjika shavu. Nilijua ni hivyo.”


PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Saunders, Saunders Kufanyiwa Upasuaji Baada ya Kupigwa na Canelo, Meridianbet

CHEZA HAPA

9 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa