Soka: Bale na Ronaldo Warejea Kwa Kishindo

Baada ya kutosikika kwenye masikio ya wapenda soka kwa muda kidogo, hatimaye Bale na Ronaldo wamerejea katika nafasi zao kwa kuzifumania nyavu wikiendi hii.

Gareth Bale alikuwa kwenye kifungo huru ndani ya kikosi cha Real Madrid kabla ya kupata nafasi ya kusajiliwa Tottenham. Hii ilimfanya ateke vichwa vya habari kila kona ya ulimwengu na wapenzi wa soka kupata nafasi ya kumuona tena uwanjani.

Japo alikaa nje kwa muda kidogo, hatimaye alirejea uwanjani na wikiendi hii amepachika goli katika mchezo dhidi ya Brighton Albion na kuisaidia Tottenham kuibuka na ushindi wa magoli 2-1.

Gareth Bale Akipachika goli la ushindi kwa Tottenham dhidi ya Brighton Albion.

Kwingineko kwenye ulimwengu wa soka, tuitizame Ligi ya Italia – Serie A. Siku kadhaa zilizopita, Cristiano Ronaldo aliripotiwa kupata maambukizi ya COVID19 na hivyo alizikosa mechi kadhaa za Serie A pamoja na kipigo kutoka kwa Barcelona kwenye Ligi ya Mabingwa.

Ronaldo alirejea uwanjani wikiendi hii katika mchezo dhidi ya Spezia. Akicheza akitokea benchi, Ronaldo alipachika magoli mawili katika ushindi wa 4-1 kwa miamba ya soka la Italia – Juventus.

Cristiano Ronaldo akipachika goli kwa mkwaju wa penati.

Kuimarika kwa kiwango cha Bale ndani ya kikosi cha Tottenham huenda kukaisaidia timu hiyo kufanya vizuri msimu huu. Upande wa pili, kurejea kwa Ronaldo ni habari njema kwa Pirlo kwani shujaa wake ataendelea kuisaidia timu hiyo kupata matokeo hasa kwenye Ligi ya Mabingwa.


Ushujaa Unakulipa Hapa!

Hii ni halisi kwa ajili ya mashujaa wote! Ukiwa jasiri unavuna mkwanja kibao hapa na sloti hii ya Huangdi Casino. Waka nusu tukupe maradufu!

Ingia Mchezoni!

22 Komentara

    Safi sana Wote Nawakubali

    Jibu

    bale bado hanaonesha maajadu yake

    Jibu

    Wako vizuri

    Jibu

    Bale aongeze juhudi ili aweze kufanya maajabu yake

    Jibu

    Habari njema kwa vilabu hivyo viwili

    Jibu

    Safi San hiy Ni habar nzur

    Jibu

    Vizuri sana

    Jibu

    Safi sana tumefurahi sana mashabiki kusikia mmerudi tena uwanjani

    Jibu

    Safii sana tunaona sasa matunda ya bale pale real Madrid walikuwq wanampotezea mafanikio yake tu .Ronald tulijua tu huyo mzee wakazi anahasira na nyavu no muda wake sasa kuziona Mara kwa Mara kuiwekea timu yake nafasi nzuri

    Jibu

    Bale na ronaldo naona walipania huo mchezo tuone mechi zijazo kama watafanya vizuri

    Jibu

    Wote wako vizur

    Jibu

    Nawakubali sana hawa jamaa Safi sana

    Jibu

    Hawa watu ni balaa

    Jibu

    Wako vizuri sana

    Jibu

    Miamba hii

    Jibu

    Vijana wako vizuri kama bale inaelekea alikua na habu na nyavu madrid walimuweka sana bench

    Jibu

    Cr7 na bale hits in town

    Jibu

    Safii sana

    Jibu

    Wote wakali

    Jibu

    Wote wapo vzuri

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Wantisha san

    Jibu

Acha ujumbe