Kocha mkuu wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amekiri kwamba Donny va de Beek aliyesajiliwa majira ya kiangazi hana furaha huko Old Trafford kutokana na kukosa muda wa kucheza.

Solskjaer Akiri Van de Beek Hana Furaha United.

Mchezaji huyo wa Umri wa 23 alisajiliwa akitokea klabu ya Ajax na alilengwa kuchukua jukumu la kiungo katika timu ya Manchester United,lakini amekuwa na wakati mgumu baada ya nafasi hiyo kuwa na wachezaji wengi wanaofanya vizuri.

Van de Beek amejumuishwa kwenye michezo 21 msimu huu nakucheza mara 10 pekee katika Premier League na ni michezo miwili pekee aliyocheza kwa kuanza.

Manchester United wapo kileleni katika ligi ya Premia wakiwa wamepata msaada mkubwa kutoka kwa wachezaji kama Fred, McTominay, Paul Pogba na Bruno Fernandes .

Kwa hali hiyo imemuacha Muholanzi huyo kukosa nafasi ya kucheza na kocha wake amekiri kukosa muda wa kucheza kwake hakumfanyi kumefanya asiwe na furaha.

“Nisingependa kusema kwamba Donny anafuraha,”Solskjaer alisema . “Ni kweli anataka kucheza zaidi lakini kumekuwa na ushindani mkali sana.

“Tunafanya vizuri na tuna wachezaji wazuri wenye kuzitendea haki nafasi wanazo cheza.”

Kulekea mchezo wa FA Cup dhid ya Liverpool, Solskjaer amesema kwamba Van de Beek atahusika katika mchezo huo utakaopigwa katika dimba la Old Trafford.

“Atacheza dhidi ya Liverpool na naweza kuleta madhara kwa upande wa timu ya Klopp,” alisema Solskjaer.


USHINDI UPI NI MKUBWA KWAKO, £2,000,000? 🤑

Pokea mualiko wa Meridianbet na Pragmatic Play kutengeneza mkwanja kwenye kasino ya mtandaoni sasa. Jiunge sasa kupata ishindi huu.

Solskjaer, Solskjaer Akiri Van de Beek Hana Furaha United., Meridianbet

INGIA MCHEZONI

18 MAONI

  1. Van de Beek kwasasa anatakiwa ajikite zaidi katika mazoezi na kusoma ligi ili atakapopata namba na muda mwingi wa kucheza aweze kuimiri mikikimikiki ya EPL na kuonyesha uwezo wake zaidi

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa