Mshambuliaji wa Roma Tammy Abraham amesema anajihisi viuzri kuichezea klabu kama Roma baada ya klabu hiyo kuvunja rekodi ya kufunga mabao mengi ndani ya msimu mmoja.
Mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea alitua Roma wakati wa dirisha la usajili la majira ya kiangazi kwa dau la £34m na tayari ameweka kambani mabao 15 kwenye ligi ya Serie A msimu huu wakati pia akicheka na nyavu mara 11 katika michuano ya Uefa Conference League.
Akiongea na midea katika utambulisho wake kwenye soka la Kiitalia Abraham alielezea furaha yake katika msimu wa kwanza na kusema ni kama “Ndoto kukamilika”
“Kukifanya hiki ninachofanya kwa klabu kubwa kama Roma kiukweli siwezi kuelezea hisia hiyo” Alisema Tammy
“Unajua kutoka kwenye msimu mgumu na Chelsea kukosa muda mwingi wa kucheza mpaka kuja hapa na kung’aa tena ni kama ndoto kuwa kweli.”