Tetesi za soka barani Ulaya leo Alhamisi 15 Aprili 2021 zinasema:-

Tetesi zinasema, Kiungo England Jesse Lingard, 28, hajaamua kuhusu ikiwa anataka kurejea Manchester United baada ya kucheza vyema kwa mkataba wa mkopo West Ham.

Tetesi zinasema, Mchezaji wa safu ya kati wa West Ham na England Declan Rice, 22, anataka kujiunga na Manchester United.

Tetesi zinasema, Mlindalango wa Arsenal na Ujerumani Bernd Leno, 29, anasema “yuko wazi kwa mapya ” na kwamba hapajawa na mazungumzo ya kurefusha mkataba wake na Gunners.

Tetesi za soka - Man

Tetesi zinasema, Mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Braut Haaland, 20, ni mchezaji anayelengwa zaidi na Barcelona kwa sasa.Timu hiyo ya ligi ya Uhispania ingependa kusaini mkataba nae katika msimu wa kiangazi lakini itasubiri mwaka ujao kama kutakuwa na haja ya kufanya.

Tetesi zinasema, Barcelona wanaamini kuwa watakamilisha mkataba wa uhamisho wa kiungo wa Manchester City na Uhispania Eric Garcia, 20, kufikia mwisho wa mwezi Aprili.

Tetesi zinasema, Juventus inataka kusaini upya mkataba na mshambuliaji wa Everton na Italia Moise Kean, ambaye yuko katika mkataba na Paris St-Germain. The Toffees wanataka euro milioni 50 (£43.5m) kwa ajili ya Kean, 21, au mkataba wa kubadilishana wachezaji unaomuhusisha kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot, 26, au kiungo wa kati-nyuma wa Uturiki Merih Demiral, 23.

Tetesi za soka - MancityTetesi zinasema, Winga wa Everton Mbrazili Bernard, 28, anasakwa na meneja wa klabu ya Real Betis Manuel Pellegrini.

Tetesi zinasema, Aston Villa wameiambia Chelsea kuwa hawana haja na mkataba wa kudumu na kiungo wa kati wa England Ross Barkley ambaye kwa sasa ana mkataba wa deni. West Ham wana nia ya kusaini mkataba na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27.

Tetesi zinasema, Liverpool wanaweza kusaini mkataba na kiungo wa kati wa Rennes na Ufaransa Eduardo Camavinga, 18, msimu huu kukaba nafasi ya mchezaji wa kimataifa wa Uholanzi Georginio Wijnaldum, 30, ambaye yuko tayari kuondoka wakati mkataba wake utakapokwisha.

Tetesi zinasema, Manchester United, Chelsea na Tottenham zote zinamfuatilia kwa karibu mshambuliaji wa Torino na Italia Andrea Belotti, 27.


JILIPE KWA NAMBA ZAKO ZA BAHATI NA KENO

Kila mtu ana namba zake za bahati, Meridianbet tunatambua namba zinaweza kukufanya milionea leo. Jilipe kwa namba zako za bahati kila baada ya dakika tano.

tetesi za soka, Tetesi za Soka Barani Ulaya, Meridianbet

CHEZA HAPA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa