Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumanne Mei 11, 2021 zinasema:-

Tetesi zinasema, Mchezaji wa timu ya taifa ya England na klabu ya Borussia Dortmund Jadon Sancho, 21, si mchezaji wa kipaumbele cha usajili kwa klabu ya Manchester United – na kuibuka kwa mchezaji Mason Greenwood ni moja ya sababu ya United kufikia maamuzi hayo.

Tetesi zinasema, Kipaumbele cha usajili kwa Arsenal mwishoni mwa msimu huu ni kiungo Eduardo Camavinga, 18, ambaye anachezea klabu ya Rennes.

Tetesi zinasema, Arsenal pia bado wana nia ya kumsajili kiungo wa klabu ya Borussia Monchengladbach na taifa la Uswizi Denis Zakaria, 24.
Tetesi za soka- sanchezMwakilishi wa kiungo wa Aston Villa na timu ya taia ya England Jack Grealish, 25, anasema kuna klabu nyingi ambazo zina mpango wa kumsajili nyota huyo.

Klabu ya AC Milan inataka kumsajili beki Fikayo Tomori, 23, kwa mkataba wa kudumu. Beki huyo wa kati kutoka England kwa sasa yupo Milan kwa mkopo akitokea Chelsea.

Kusajili mshambuliaji ndio kipaumbele namba moja kwa Barcelona mwisho wa msimu huu ambapo mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Braut Haaland, 20, ndio chaguo lao la kwanza huku mshambuliaji wa Manchester City na Argentina Sergio Aguero, 32, akiwa ni mbadala.
Tetesi za soka - WillockTetesi zinasema, Klabu ya Tottenham Hotspur inapanga kumuuza beki wa kati wa Colombia Davinson Sanchez, 24, mwishoni mwa msimu.

Tetesi zinasema, Golikipa raia wa Ujerumani, Bernd Leno, 29, na beki wa kulia kutoka Uhispania Hector Bellerin, 26, ni miongoi mwa wachezaji sita ambao Arsenal watawaingiza sokoni kuwauza mwishoni mwa msimu.

Tetesi zinasema, Newcastle United wanataka kumsajili winga Joe Willock, 21, kutoka Arsenal kwa mkataba wa kudumu. Wilock amelivutia benci la ufundi la Newcastle ambako anacheza kwa mkopo.


PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

tetesi za soka, Tetesi za Soka Barani Ulaya, Meridianbet

CHEZA HAPA

5 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa