Tetesi za soka barani ulaya leo Alhamisi Mei 13, 2021 zinasema:-
Tetesi zinasema, kocha wa zamani wa Chelsea Frank Lampard ndiye anayeonekana kuwa mtu sahihi wa kuchukua nafasi ya Roy Hodgson katika klabu ya Crystal Palace. Mkataba wa Hodgson ambaye pia ni kocha waw zamani wa England unamalizika mwisho wa msimu huu. 

Afisa mkuu mtendaji wa Borussia Dortmund Hans-Joachim Watzke amesema mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland, 20 , atasalia katika klabu hiyo msimu ujao.

Barcelona wamewasiliana na wawakilishi wa kocha wa Bayern Munich Hansi Flick, huu kukiwa na mashaka juu ya mustakabali wa hatma ya kocha wa sasa Ronald Koeman katika klabu hiyo.
Tetesi za soka.
Barcelona wamefanya mawasiliano na golikipa wa Juventus Mkongwe Gianluigi Buffon, ambae ataachana na vibibi vizee hao wa Turin, mwishoni mwa msimu

Afisa mkuu mtendaji ajaye wa Bayern Munich Oliver Kahn ametaja hatua yoyote ya uhamisho wa Haaland ni “isiyofikirika” kwa sababu ya ada ya zaidi ya euro millioni 100 sawa na (£85m) ambayo inazungumziwa.

Winga wa Dortmund na England Jadon Sancho, 21, anamshinikiza wakala wake kufanikisha uhamisho wake kwenda Manchester United baada uhaimisho huo kugonga mwamba msimu uliopita.
Tetesi za soka.
Manchester United wanavutiwa na mlinzi wa Atalanta Muargentina Cristian Romero, 23, ambaye ameungana na mlinzi wa Lille aliye na umri wa miaka 21- Mholanzi Sven Botman na mchezaji wa Sevilla Jules Kounde, 22 , katika orodha ya wachezaji wanaosakwa na klabu hiyo ya Ligi ya England.

Kocha wa zamani wa Bournemouth Eddie Howe amekubali kuwa meneja mpya wa Celtic.

Tottenham wanajiandaa kuanza usajili wa kumtafuta kocha mpya katika kipindi cha siku chache zijazo. Scott Parker wa Fulham ameorodheshwa lakini klabu hiyo haijakata tamaa ya kumpata meneja wa Leicester City, Brendan Rodgers.

Mshambuliaji wa Slavia Prague aliye na umri wa miaka 19-raia wa Senegal Abdallah Sima, ambaye ananyatiwa na Arsenal na West Ham, anapania kuhamia Ligi ya England.


PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

tetesi za soka, Tetesi za Soka Barani Ulaya, Meridianbet

CHEZA HAPA 

7 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa