Tetesi za soka barani Ulaya leo tarehe Mei 27, 2021 zinasema:-

Tetesi zinasema, Kocha Zinedine Zidane ameamua kuondoka Real Madrid na tayari ameshawafahamisha wachezaji juu ya uamuzi wake siku ya Jumatano. 

Tetesi za soka - TammyTetesi zinasema, Leicester City wanakaribia kukamilisha makubaliano ya usajili wa pauni milioni 18 wa kiungo wa mabingwa wa Ligi ya Ufaransa Lille, Boubakary Soumare, 22.

Tetesi zinasema, Leicester pia wanaweza kumpa nafasi ya kusalia katika Ligi ya Premia beki wa kati wa klabu ya Schalke Mturuki Ozan Kabak, 21 – ambaye amekuwa Liverpool kwa mkopo kwa nusu ya msimu uliokamilika.

Tetesi zinasema, Borussia Dortmund inafanya mawasiliano na Chelsea juu ya uwezekano wa kuwasajili Tammy Abraham, 23, na Callum Hudson-Odoi, 20.

Tetesi zinasema, Hatua hiyo inakuja kama pigo kwa West Ham, ambao huenda wasiweze kufikia kiwango cha pauni milioni 40 ambacho Chelsea wanakitaka kwa ajili ya Abraham.

Tetesi zinasema, Wakati huo huo, nia ya Dortmund ya kumtaka Hudson-Odoi inaweza kutoa fursa kwa mshambuliaji wa England Jadon Sancho, 21, kuondoka katika klabu ya Bundesliga kuelekea Manchester United.
Tetesi za soka- soumare
Tetesi zinasema, Liverpool wamefikia makubaliano ya kumsajili beki Mfaransa Ibrahima Konate, 22, kutoka klabu ya RB Leipzig kwa mkataba wa miaka mitano.

Tetesi zinasema, Matumaini ya Livepool kumsajili kiungo wa Udinese Muargentina Rodrigo de Paul mwenye umri wa miaka 27 yameongezeka baada ya AC Milan kuachana na mpango wa kutaka kumsajili.

Tetesi zinasema, Winga wa Brazili Raphinha, 24, anasema kuwa hafikirii kuhusu kuondoka Leeds United, licha ya tetesi zinazomuhusisha na kuhamia katika klabu za Manchester United na Liverpool.
Tetesi za soka - Raphina
Tetesi zinasema, Klabu za Ligi kuu England zitatakiwa kusubiri hadi Julai kabla ya kuwasiliana na Barcelona kuhusu mipango ya kumsajili mshambuliaji Mbrazili Philippe Coutinho, 28. Arsenal na Everton wanadhaniwa kuwa wanamtaka.

Tetesi zinasema, Mlinda mlango Muingereza Sam Johnstone, 28, anasema mustakabali wake upo mikononi mwa klabu ya West Brom licha ya kuhusishwa na taarifa za kuhamia Leeds na West Ham kwa malipo ya pauni milioni 20.


BONASI YA 50% KILA SIKU KATIKA KASINO ZA EVOPLAY HAPA MERIDIANBET.

Meridianbet na Evoplay Kasino wanakupa bonasi ya 50% ya kiasi utakachoweka katika akaunti yako leo. Unasubiri nini ni wakati wa kupiga pesa sasa na Mabingwa.

tuchel, Tuchel :Tuna Bahati Tottenham Wametusaidia Kazi., Meridianbet

SOMA ZAIDI

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa