Thomas Tuchel amejaribu kueleza ni kwa nini Romelu Lukaku alibaki benchi na kutotumika  wakati Chelsea ilipochapwa 1-0 na Everton bao lililowekwa kimiani na Richarlison baada ya Azpilicueta kufanya kosa lililoigharimu timu, lakini maswali zaidi yakiulizwa kuhusu uwepo wa mshambuliaji huyo wa Ubelgiji Stamford Bridge.

Tuchel Afunguka Kwanini Hakumtumia Lukaku vs Everton

Chelsea walisafiri mpaka Goodison Park siku ya Juampili kwaajili ya mchez\o wa Premier Laegue kuchuana na Everton ambao wanapambana kuepuka kushuka daraja wakati huohuo The Blues walikuwa kutafuta kujisimika kumaliza nne za juu.

Tuchel aliamua kutomuanzisha mshambuliaji Romelu Lukaku wakati kikosi chake kilipohitaji msukumo wa kushambulia kipindi cha pili Merseyside.

Lakini aliamua kuwaingiza Christian Pulisic na Hakim Ziyech wakati akisaka bao la kusawazisha na aliwaambia waandishi wa habari baadaye alipoulizwa kwa nini Lukaku alibaki kwenye benchi: “Kwa sababu tulimtoa Jorginho. Tulikuwa na mabadiliko matatu tu.”

Chelsea, ambayo imeshuhudia Lukaku akishindwa kufunga bao la Ligi Kuu tangu Desemba 29, itarejea uwanjani wikendi ijayo itakapocheza na Wolves.

WEKA MKEKA WAKO HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa