Kocha mkuu wa timu ya Chelsea Thomas Tuchel amewaambia waandishi kwamba hajali kuhusu mawindo ya mataji kwa Liverpool msimu huu.

Liverpool wapo katika nafasi kubwa ya mbio za ubingwa wa EPL, pia wametinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa lakini tayari wametwaa taji la Carabao kwa kuifunga Chelsea kwenye mikwaju ya penati.

Chelsea wataumana na Liverpool katika fainali ya FA Cup mwezi Mei 14 katika uwanja wa Wembley na hii inakuwa fainali ya tatu mfululizo kwa Chelsea katika michuano hiyo na kupoteza kwa Arsenal 2020, wakapoteza kwa Leicester Cuty 2021  na sasa Liverpool.

“Sijali kuhusu mataji mengine ya Liverpool,” alisema kocha huyo wa The Blues

“Ndiyo tulipoteza Carabao Cup tulifanya kila kitu lakini bahati haikuwa kwetu kama mnavyo jua mpaka tulipokosa penati ya mwisho.

“Tutajiandaa vyema dhidi ya timu imara ulimwenguni kwa sasa, itakuwa mechi ngumu na tutajaribu kufanya maisha yawe magumu kwao.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa