Mashabiki wa Manchester United walisababisha mchezo huu uhairishwe Mei 2 baada ya kuvamia uwanja kwa kile walichodai ni maandamano ya kumtaka mmiliki wa klabu hiyo awaachie timu yao kufuatia timu kuwa na muenendo mbaya na kujiunga na Super League.

Uchambuzi EPL: Manchester United vs Liverpool

Taarifa za Vikosi:

Kocha wa United Ole Gunnar Solskjaer anatarajia kukibadili kikosi chake cha kwanza baada ya kufanya mabadiliko kwenye mchezo dhidi ya Leicester.

Nahodha Harry Maguire atakosa mechi ya leo kwa mara nyingine kutokana na tatizo la kifundo cha mguu na atakuwa akipambana kuona kama atahusika katika fainali ya Europa League Mei 26 dhidi ya Villarreal.

Wachezaji wa Liverpool Ozan Kabak, Naby Keita, James Milner na Ben Davies wote pia watakosa mchezo huu sababu ya majeraha madogo.

Divock Origi na Caoimhin  Kelleher wamerejea mazoezini.

Rekodi za Kukutana:

Manchester United wamepoteza mchezo mmoja kati ya 15 ya nyumbani dhidi ya Liverpool katika mashindano yote (W10,D4) na hawajafungwa katika michezo nane.

Nyumbani na Ugenini United imeshinda mara moja pekee katika michezo 9 ya ligi (D6,L2).

Manchester United imepoteza michezo mitano ya nyumbani katika Premier League msimu huu idadi kubwa zaidi katika misimu miwili iliyopita.

Liverpool imeshinda mechi mbili za katikati ya wiki katika Premier League msimu huu na ushindi wote walipta dhidi ya Tottenham.

Firminho amefunga Man United goli moja kati ya 14 wakati pia Sadio Mane amefanikiwa kufunga bao moja katika michezo 11 dhidi ya Red Divels.

Kikosi cha Manchester United Kinachoweza Kuanza (4-2-3-1): Henderson; Wan-Bissaka, Bailly, Lindelof, Shaw; McTominay, Fred; Rashford, Fernandes, Pogba; Cavani

Kikosi cha Liverpool Kinachoweza Kuanza (4-3-3): Alisson; Alexander-Arnold, Phillips, Williams, Robertson; Thiago, Fabinho, Wijnaldum; Salah, Firmino, Mane


PESA IPO HAKinachoweza Kuanza:PA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

manchester united, Uchambuzi EPL: Manchester United vs Liverpool, Meridianbet

CHEZA HAPA

13 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa