Timu 9 kati ya 12 za Super League zimethibitisha kujitolea kwao kwa UEFA na kukataa mpango wa kuunda mashindano mapya, lakini zitakabiliwa na adhabu ya kifedha kutoka kwa shirikisho la mpira wa miguu la Ulaya.

UEFA Yazirudisha Timu 9 Zilizo Jaribu Kujiunga na Super League

Timu tatu ambazo ni Barcelona, ​​Real Madrid na Juventus zimekataa kuunganishwa tena na UEFA na zitakabiliwa na adhabu zaidi.

Njama ya kuunda Ligi Kuu mpya ilibuma siku chache tu baada ya kutangazwa kwa kuundwa kwake, na timu nyingi zilijiondoa kufuatia vitisho kutoka kwa vyama vya mpira wa miguu na maandamano ya mashabiki.

Licha ya kukataa mpango huo, timu tisa zilizorejeshwa tena – Arsenal, AC Milan, Chelsea, Atletico Madrid, Inter, Liverpool, Manchester City, Manchester United na Tottenham – zitapoteza asilimia tano ya mapato ambayo wangepata kutoka UEFA kwa msimu mmoja.

“Klabu hizo tisa zimekubali mpango wa Super League ulikuwa makosa na wameomba radhi kwa mashabiki, vyama vya mpira, ligi za kitaifa, vilabu vya Ulaya na UEFA,” taarifa kutoka UEFA ilisomeka hivyo.

“Pia wametambua kuwa mradi huo usingeidhinishwa chini ya Kanuni za UEFA.”

Klabu hizo zitakabiliwa na faini ya Euro 100 milioni (£ 87m / $ 122m) ikiwa watajaribu kucheza kwenye mashindano mengine yasiyoruhusiwa kama Super League.


ENGENEZA FAIDA KUPITIA MCHEZO WA TITAN DICE UKIWA NA MERIDIANBET KASINO

Unapokuwa kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, huna sababu ya kucheza kwa mashaka. Titan Dice, ni mchezo unaweza kukupatia mamilioni kwa mzunguko mmoja!

uefa, UEFA Yazirudisha Timu 9 Zilizo Jaribu Kujiunga na Super League, Meridianbet

SOMA ZAIDI

7 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa