Ufaransa ndiyo taifa linalopewa nafasi kubwa ya kushinda Mashindano ya Ulaya msimu huu wa joto, lakini kuna machafuko katika kikosi cha Les Bleus baada ya Kylian Mbappe kutokubaliana na maoni yaliyotolewa na Olivier Giroud.

Ufaransa: Hali si Shwari Sana kwa Mbappe na Giroud

Mshambuliaji huyo wa Chelsea alitoka benchi na kufunga mabao mawili ya mwisho katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Bulgaria, lakini alipoulizwa na mwandishi wa habari juu ya kiwangochake cha utulivu alijibu waziwazi.

“Unasema kwamba nilikuwa kimya, lakini ni kwa sababu wakati mwingine ninaomba mpira na haufiki kwangu,” Giroud alisema.

“Halafu, ninajaribu kuomba mara nyingi kwa wachezaji wenzangu na kujaribu kutoa maamuzi kwenye lango la upinzani.”

Kwa mujibu wa L’Equipe, Mbappe alihisi kutengwa na maoni ya Giroud, haswa wakati mchezaji huyo wa miaka 34 alionyesha misaada iliyotolewa na Benjamin Pavard na Wissam Ben Yedder.

“Nikiwa na usaidizi mzuri kutoka kwa Ben Yedder na Pavard, niliweza kumaliza mchezo vizuri, lakini tungeweza kufunga mabao mengi ikiwa tungekuwa na ufanisi zaidi,” Giroud aliongeza.

Ufaransa, Ufaransa: Hali si Shwari Sana kwa Mbappe na Giroud, Meridianbet

Giroud aliomba msamaha kwa Mbappe baada ya chakula cha mchana katika kituo cha mafunzo cha Ufaransa, lakini ripoti huko Ufaransa zinasema kuwa kijana huyo wa miaka 22 hakuridhika na akamwambia bosi wa Les Bleus Didier Deschamps kwamba anataka kufanya mkutano na waandishi wa habari siku ya Alhamisi kuelezea upande wake wa hadithi. .

Lakini, Deschamps alimuondoa Mbappe, akamtuliza na kumwambia azingatie mchezo wa ufunguzi wa Ufaransa wa Euro 2020 dhidi ya Ujerumani Jumanne, Juni 15.

Maoni yaliyotolewa na Giroud, wanasema L’Equipe, hayajaathiri timu lakini yameacha hisia tofauti kwa Mbappe, ambaye hafurahii hali yote.


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

5 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa