Van Gaal: Ten Hag Kuwa Makini Man United ni Klabu ya Biashara

Kocha wa timu ya taifa ya Uholanzi Louis van Gaal amemuonya bosi wa Ajax Erik ten Hag kuhusu kuchukua majukumu ya kuinoa klabu ya Manchester United.

Van Gaal: Ten Hag Kuwa Makini Man United ni Klabu ya Biashara
Erik ten Hag

Ten Hag mwenye umri wa miaka 52 alikutana na mabosi wa Manchester United wiki iliyopita kuongelea kuhusu kocha wao mpya ajaye na imeonekana kama Ten Hag yupo kwenye nafasi kubwa ya kuyabeba majukumu hayo makubwa wakati wa majira ya kiangazi.

Van Gaal ambaye aliwahi kuifundisha Manchester United mwaka 2014 na 2016 amemuonya Ten kwamba ajiunge na klabu ya mpira wa miguu sio klabu ya Kibishara.

“Nafikiri Erik ten Hag ni kocha mzuri, ameonyesha hivyo mara kadhaa”, alisema van Gaal, kwa gazeti la Uholanzi AD.

“Manchester United ni klabu ya kibiashara na hayo ni maamuzi magumu kwa kocha. Ni bora kwenda kwenye klabu ya soka. Sitasimamia kazi yake na ataniita mwenyewe. Lakini anapaswa kuchagua klabu ya soka, si klabu ya kibiashara.”


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

Acha ujumbe