Wakala wa beki wa Chelsea Antonio Rudger alikutana na uongozi wa klabu ya Barcelona kwaajili ya uwezekano wa uhamisho wa kujiunga na klabu hiyo wakati wa majira ya kiangazi.

Wakala wa Rudger Akutana na Uongozi wa Barcelona

Mshauri huyo wa Rudger Sahr Senesie alikutana na mkurugenzi wa michezo wa Barca Mateu Alemany na msaidizi wake Jordi Cruyff kwa mazungumzo kwenye moja ya mgahawa huko Barcelona.

Kikao hicho kilichukua masaa matatu ambapo walikaa pamoja wakinywa wine na maji na miamba hao huenda wakamsajili mlinzi huyo kwa uhamisho wa bure.

Rudger anaelekea kumaliza mkataba wake na The Blues mwisho wa msimu huu hali hiyo inamruhusu kuanza mazungumzo na vilabu vya nje ya Uingereza lakini wakala wake anaendelea kufanya mazungumzo na vilabu kama Real Madrid na Paris Saint-Germain.


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa