Kwa mara ya 5 kwenye historia ya EPL, klabu ya West Brom Albion wanashuka daraja msimu huu.
Magoli 3 ya vijana wa Arteta kutoka kwa Emil Smith Rowe ambaye amefunga goli la kwanza kwenye EPL akiwa na klabu ya Arsenal, Nicolas Pepe na Willian yalitosha kuzamisha jahazi la Sam Allardyce ambaye anahitaji pointi 10 ili kubaki EPL msimu ujao.
Kimahesabu, West Brom wameshashuka daraja kwani zimesalia mechi 3 pekee msimu huu kukamilika na hivyo pointi 1 pungufu, inawafanya waporomoke na daraja na msimu ujao watacheza ligi ya Championship.

Licha ya Costa Pereira kuendelea kuwa mhimili wa Big Sam, kocha huyu anaandika historia ya kushuka daraja kwa mara ya kwanza tangu awe kocha wa vilabu mbalimbali vya EPL.
Hakika siku ya kufa nyani, miti yote huteleza. Big Sam kwa mara ya kwanza anakwenda kuifundisha klabu ya Championship akiwa ameshuka nayo daraja kutoka EPL.
Ushindi kwa Arsenal, unawapa matumaini vijana wa Mikel Arteta huenda wakapa nafasi ya kucheza Mashindano ya Europa msimu ujao kama wataendelea kupata matokeo chanya kwenye michezo 3 ya EPL iliyosalia msimu huu.
Kupoteza mchezo dhidi ya Arsenal, kunawafanya West Brom Albion kuungana na Sheffield United katika orodha ya timu 3 zinazoshuka daraja msimu huu. Leo ni Fulham vs Burnley, Fulham akipoteza mchezo huu ataungana na timu hizi katika orodha ya wanaoshuka daraja na Burnley atakuwa amejihakikishia kusalia EPL msimu ujao.
Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.
Duh,pole yao
Pole yao
Acha washuke daraja
Poleni sana
Pole sana
Pole yao
Hii sio poa kabisaa
Wajipange tena vizuri
Pole yao
Wajipange upya
Pole yao