Kocha wa Barcelona Xavi Hernandez amekerwa na timu yake kushindwa kuitumia vyema nafasi ya kipekee kujihakikishia nafasi ya pili katika msimamo wa Liliga baada ya timu hiyo kukubali kipigo cha 1-0 katika uwanja wa Camp Nou.

Barca wamepoteza katika uwanja wa nyumbani mfululizo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2003, walipoteza dhidi ya Frankfurt na kuondolewa katika michuano ya Europa League siku tano kabla ya kuumana na Cadiz katika Laliga.

Kwa matokeo hayo Xavi amekiri kuondoa matumaini ya ubingwa baada ya kuachwa alama 15 na vinara Real Madrid licha ya kuwa na mchezo mkononi na amesema hilo halikubaliki lazima wachezaji waonyeshe kiu ya ushindi.

“Tuna hasira. Tumepoteza nafasi nzuri sana, ya dhahabu, kujitofautisha na timu za Ligi ya Mabingwa na kwa kweli tunaaga ligi,” Xavi aliwaambia waandishi wa habari baada ya mechi.

“Nina hasira, tunatakiwa kucheza kwa kujituma zaidi, tunatakiwa kufanya mambo mengi zaidi, tumejizoeza kwa hili, mimi ndiye ninayewajibika zaidi, tulipaswa kuonyesha ari zaidi.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa