Xavi Hernandez amechagua kuongeza muda wake wa kukaa katika kikosi cha Al-Sadd cha Qatar kwa miaka mingine miwili, klabu yake ilisema siku ya Jumatano, na kupunguza uvumi kwamba angeweza kutua katika klabu yake ya zamani ya Barcelona kwa msimu ujao.
Kiungo huyo wa kati wa zamani alijiunga na Al-Sadd kama mchezaji mwaka 2015 baada ya miaka 17 ya kubeba mataji na Barca, na sasa ni kocha mkuu baada ya kutundika daruga mwaka 2019. Mwezi uliopita aliongoza timu hiyo kutwaa taji la ligi ya ndani ya Qatar huku akiwa bado hajafungwa.
Xavi aliikataa nafasi ya kuwafundisha Wakatalunya mwezi Januari 2020 baada ya Ernesto Valverde kufungashwa virago na ameendelea kuhusishwa na kwenda huko Camp Nou, hata tangu Ronald Koeman alipochukua nafasi ya Quique Setien Agosti iliyopita.
Hatima ya Koeman huko Barca bado imegubikwa na sintofahamu baada ya kampeni ngumu na kutokana na makubaliano mapya ya Xavi na Al-Sadd inamaanisha kuwa Mholanzi huyo hana haja ya kuwa na wasiwasi juu ya kiungo wa zamani wa Uhispania kuja kuchukua nafasi yake hivi karibuni.
Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.
Bonge la dili pongezi kwake
Deal done!!
Hongera zake na kazi iendelee
Hapa kazi tu hongera sana
Bonge la dili
Kazi tuuu
Safi
Dili nene