YANGA: Namungo Sio Wepesi

Uongozi wa Yanga umesema kuwa mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo FC hautakuwa mwepesi ila wapo tayari kwa ajili ya ushindani ili kupata pointi tatu muhimu. 

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi ina kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Namungo FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Hemed Morocco.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na nafasi za timu zote mbili ndani ya ligi.

Namungo inapambana kubaki ndani ya ligi huku Yanga hesabu zao ikiwa ni kutimiza jambo lao la kutwaa ubingwa ulio mikononi mwa Simba.

Yanga

Mchezo wao wa mzunguko wa kwanza walipokutana Uwanja wa Mkapa, ubao ulisoma Yanga 1-1 Namungo, ambapo Bigirimana Blaise alikosa penalti baada ya kipa Metacha Mnata kuokoa.

Senzo Mazingiza ambaye ni Mjumbe wa Kamati kuelekea katika mabadiliko ndani ya Yanga amesema kuwa wapinzani wao sio wa kuwabeza.

Yanga

Namungo ni timu imara hivyo mchezo wetu hautakuwa rahisi ila kutokana na kikosi tulicho nacho pamoja na mbinu za mwalimu kuna jambo la tofauti linaweza kutokea.

“Kikubwa ambacho tunahitaji ni kuona kwamba tupata matokeo kwa kuwa wachezaji wapo tayari kupambana na kupata ushindi,”.

Kwenye msimamo wa ligi, Yanga ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 57 baada ya kucheza jumla ya mechi 27 inakutana na Namungo FC iliyo nafasi 11 na pointi 32.


PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

CHEZA HAPA

8 Komentara

    Namungo wako vizuri yanga wajipange

    Jibu

    Ongezeni bidii yanga na wala asiwe woga

    Jibu

    Namungo sio ya mchezo yanga watatoka kweli

    Jibu

    Yanga ubingwa wenu

    Jibu

    Yanga wajipange msiogope huu ni mpira lolote linaweza tokea mkashinda

    Jibu

    Tena yanga wajipange sana

    Jibu

    Yanga wajipange sana kwa namungo

    Jibu

    Yanga wajipange

    Jibu

Acha ujumbe