Yanga kufanya sherehe ya Unbeaten kesho

Baada ya kuweka rekodi ya kutofungwa katika michezo 49 ya ligi kuu, Uongozi wa Yanga umeweka wazi kwamba watafanya sherehe kesho.

 

Sherehe hizo zitafanyika kesho jumapili kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar ambapo kikosi hicho kitakuwa kikimenyana na Tanzania Prisons.

Akizungumzia mipango hiyo, Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema “Kesho tutakuwa na sherehe za kusherehekea kutofungwa mechi 49 za ligi.

“Sherehe hizo tutazifanya kwenye Uwanja wa Mkapa kabla ya mechi yetu dhidi ya Tanzania Prisons na tutaanza kufanya saa 8:00 mchana mpaka muda wa mchezo.

“Tutaifanya kama nusu ya siku ya Mwananchi, watakuwepo wasanii mbalimbali kwa ajili ya kutoa burudani kwa mashabiki wetu.”

Acha ujumbe