Kiungo wa Lazio Daniel Guerini amefariki akiwa na umri wa miaka 19 na kuacha wasoka la Italia likiomboleza.

Daniel Guerini Afariki Kwa Ajali ya Gari

Gazzetta dello Sport ni moja chanzo cha habari ambacho kimeripoti kwamba kinda huyo aliuawa kwenye ajali ya gari huko Roma siku ya Jumatano.

Guerini, alikuwa ni sehemu ya kikosi cha Lazio cha U19 alitumia muda wake na Torino, Fiorentina na SPAL kabla hajahamia katika huko Stadio Olimpico.

Taarifa ya Lazio ilisomeka: “Bado ni ajabu na mshangao mkubwa na maumivu kwa Rais, wanawake na wanaume wa Lazio Sports Club pamoja na familia ya kijana Daniel Guerini.’

Fiorentina waliweka ujumbe: “Tumeshitushwa na kusikitishwa kupata taarifa za kifo cha mchezaji kijana wa Lazio Daniel Guerini, ambaye aliwahi kuwa ni mchezaji katika akademi ya Fiorentina mwaka 2018-2019 na 2019-20.

“Kwa pamoja rais Cammisso na kila mtu hapa tupo pamoja na familia ya Guerini katika kipindi hiki kigumu.

Torino waliandika katika kurasa zao: “Rais Urbano Cairo na klabu nzima ya Torino tumeshangazwa na tuna masikitiko makubwa kwa kifo cha Daniel Guerini ambaye amewahi kuwa ni mchezaji wetu wa Primavera.”

Mchezaji huyo ambaye alianza kuichezea timu ya vijana ya Lazio kabla hajajiunga na Torino mwaka 2016.

Na alirejea tena Lazio mwezi Januari akiwa na mkatab wa miaka mitatu baada ya kukupita katika vilabu vya Fiorentina na kutumia mwaka mzima na SPAL.


Maana Kamili ya Ushindi Katika Kasino za Meridianbeti ni Pamoja na Mchezo wa Tropical Wild.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Tropical Wild na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Daniel, Daniel Guerini Afariki Kwa Ajali ya Gari, Meridianbet

CHEZA

6 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa