David Alaba anatarajia kusaini mkataba rasmi na Real Madrid mwezi Mei.

Nyota huyu mwenye uraia wa Austria, amekuwa akihusishwa na uhamisho kwenda vilabu kadhaa msimu huu, wakati mkataba wake wa sasa na Bayern Munich ukiwa mbioni kufika tamati mwisho wa mwezi Juni.

Licha ya klabu kadhaa kuhusishwa na saini ya staa huyu mwenye miaka 28, kwa mujibu wa mwanahabari Fabrizio Romano, Madrid wamekuwa mbele kwenye mbio hizi tangia mwezi Januari.

David Alaba Akubaliana Miaka 4 na Real Madrid!

Taarifa zinasema kuwa, Chelsea, Paris Saint-Germain, Liverpool na Barcelona wameshindwa kumshawishi staa huyu, huku upande wa Zidane ukiwa na nafasi nzuri zaidi.

Staa huyu anatajwa kuwa mwezi Mei nyota huyu anatarajia kusaini mkataba na Real Madrid, na anaonekana ataweza kuziba pengo la Sergio Ramos, ambaye mpaka sasa bado hajakubali kusaini mkataba mwingine pale Bernabeu.

Alaba, kwa mara nyingine amekuwa mchezaji muhimu sana kwenye kikosi cha Bayern msimu huu, akifunga magoli magoli mawili na kutoa asisti tano kwenye mechi 42 alizocheza za michuano yote.


 

KWANI MERIDIANBET WANASEMAJE! MKWANJA UPO KWENYE KASINO MPYA YA MINI POWER ROULETTE.

Unawezaje kukosa ubingwa ndani ya kasino hii maridhawa, Nafasi ya kushinda mkwanja ni kwa kila mtu, Meridianbet inakupa nafasi ya kuwa mmoja ya washidi leo, unasubiri nini?

Mini Power Roullete

CHEZA HAPA

15 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa