Manchester City itamtathmini Kevin De Bruyne kugundua ukali wa jeraha la kiungo huyo kabla ya safari ya Jumatano Aston Villa.

De Bruyne aliumia wakati wa mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Chelsea Jumamosi na jeraha la kifundo cha mguu baada ya kugongana na N’Golo Kante.

Ilikuwa ni changamoto isiyo na hatia kutoka kwa kiungo wa Chelsea lakini De Bruyne alionekana kuumia mguu wake na hakuweza kuendelea, na Phil Foden alikuja kuchukua nafasi yake baada ya dakika 48.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji atafanyiwa vipimo jumapili lakini bosi wa City Pep Guardiola alitoa makadilio yake ya awali kuwa jeraha ni la kutisha baada ya mchezo kumalizika.

Alipoulizwa juu ya taarifa mpya, Guardiola aliiambia Manchester Evening News: “Sijui – ana maumivu.

“Jumapili tutafanya vipimo na madaktari lakini haionekani vizuri. Tutaona kesho. ”

De Bruyne alikosa michezo saba mwezi Januari na Februari kwa sababu ya jeraha la nyama ya mguu lakini, pamoja na kutokuwepo kwa michezo miwili mwaka 2019, hana historia ya shida ya kifundo cha mguu.

Amecheza mara 35 kwenye mashindano yote kwa City msimu huu, akifunga nane na kusaidia mabao 15.


JILIPE KWA NAMBA ZAKO ZA BAHATI NA KENO

Kila mtu ana namba zake za bahati, Meridianbet tunatambua namba zinaweza kukufanya milionea leo. Jilipe kwa namba zako za bahati kila baada ya dakika tano.

CHEZA HAPA

4 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa