Kufuatia kuwa na msimu wenye maneno mengi kumuhusu kipa wa Manchester UnitedDavid De Gea, sasa ameamua kujikingia kifua na kuweka wazi lengo lake la kuipigania jezi namba 1.

Kwa misimu miwili iliyopita, De Gea anaonekana kushuka kiwango kwa kufanya makosa kadhaa ambayo yameigharimu timu kwa kiasi kikubwa. Inakumbukwa mechi ya nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Chelsea, De Gea alifanya makosa mawili yaliyopekea kufungwa magoli mawili.

de gea, De Gea Ajikingia Kifua, Meridianbet

Wadau mbalimbali wa mchezo wa soka wamekuwa wakielezea hisia zao kuhusu kiwango cha De Gea,wengi wao wamekuwa wakimtaka Ole Gunnar Solskjaer kufanya maamuzi ya haraka na kumkabidhi mikoba kipa chipukizi Dean Henderson.

De Gea amenukuliwa akisema ” Ninajiamini, nimekuwa nikionesha ubora wangu kwa miaka mingi na hivyo muda wote ninapatikana kama kocha akinihitaji. Nipo tayari kucheza muda wowote na kuisaidia timu kama kawaida.”

de gea, De Gea Ajikingia Kifua, Meridianbet

Akizungumzia Mashindano ya Europa, De Gea amesema ” nadhani kiwango chetu kimeongezeka msimu huu. Tulikuwa tumezidiwa pointi 14 na timu iliyokuwa nafasi ya 3 kwenye Msimamo wa EPL lakini mwisho wa siku tumemaliza katika nafasi ya 3.

“Nadhani tumecheza vizuri kwenye michezo mingi. Kusema ukweli, tulistahili kucheza fainali. Pengine tulihitaji uzoefu zaidi kwenye kikosi na kutumia nafasi za kufunga tulizozipata. Tutaendelea kuongeza kiwango na kuipigania timu  pamoja na kushinda mataji msimu ujao.”

de gea, De Gea Ajikingia Kifua, Meridianbet

Baada ya kumaliza msimu kwa kutolewa kwenye nusu fainali ya Michuano ya Europa. Wachezaji wa Manchester United wamepatiwa likizo ya wiki 2 kabla hawajarudi tena kwenye mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao.


Drops and Wins!

Umeijua hii? Ni promosheni kabambe ya ushindi kwenye Casino ya mtandaoni ya Meridianbet! Unaweza kushinda hadi Euro 2,000,000 leo.

Soma zaidi ucheze

38 MAONI

  1. De gea wasimulaumu bure wamlaumu kocha aliepanga kikosi cha wachezaji wabovu de gea yeye kazi yake ni kudaka tu na si uchezaji

  2. Makosa yapo hakuna mtu hasiyekosea. De gea amefanya makubwa sana kwenye clabu ya man u kwa likizo waliyo mpa naamni kabisa kuna mabadiliko makubwa sana tutayaona kutoka kwake

  3. De gea yuko vizuri ingawa kuna mambo yanajitokeza lakini sio kwa kusudi naninaamini kuwa ni kila bora zaidi kama watamuacha Chelsea watamchukua tena

  4. De gea kwa msimu miwili iliyopita anaonekana kushuka kiwango kufanya makosa kazaa ktk timu ingawa ni mchezaji anayejituma sana

  5. De gea kiukwel msimu huu amezingua sana tuangalie Kama kwel ataweza kutetea jez namba 1 maana alipoangalia anapokonywa kabisa Henderson

  6. Mi naamini de gea ni kipa bora Sana na katika soka kuna makosa madogo madogo ambayo yanatokea man u wakiruhusu kumuachia watakua wamepoteza jembe.

  7. De Gea kutoka kuwa golikipa anayesifiwa hadi kujitetea , inawezekana ana tatizo jingine nje ya uwanja linaloathiri uwezo wake uwanjani#meridianbettz

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa