Hakika siku ya kufa nyani miti yote huteleza. Hii ndio hali ya David Moyes kwa nahodha wake – Declan Rice.

Rice amekuwa kwenye kiwango thabiti msimu huu na muhimili mkubwa wa mafanikio ya West Ham United msimu huu.

Ikiwa ni Michezo 30 pekee ambayo imeshachezwa kwenye EPL mpaka sasa, Declan Rice ameitumikia West Ham katika Michezo 14 kwenye Safu ya kiungo.

Kuongezeka kwa Jesse Lingard, kumeongeza ari ya timu hiyo na ikiwa ni sambamba na kumpunguzia Rice majukumu ya kushambulia na hivyo ameendelea kuwa msingi imara Kama kiungo mkabaji.

Jesse Lingard
Jesse Lingard akishangilia goli lake la 6 Akiwa na The Hammers msimu huu

David Moyes anakwenda kumkosa Rice kwa wiki 4 kufuatia mchezaji huyo kupata majeraha ya goti alipokuwa na timu ya Taifa ya Uingereza.

Kuumia kwa Rice kumefungua mlango kwa mkongwe Mark Noble ambaye aliiongoza vyema West Ham United kwenye ushindi dhidi ya Wolves (3-2) Jana usiku.

Kwa kiwango bora cha Rice msimu huu, kocha wa West Ham United alinukuliwa akisema “itahitajika benki ya Uingereza na Benki ya Scotland ili timu yeyote iweze kumsajili Declan Rice”

Swali ni; Je, Rice ataendelea kubaki West Ham United au atahitaji kwenda kwenye timu inayopambana kupata mataji kila msimu?


INAWEZEKANA KUWA MILIONEA BILA KUVUJA JASHO NA KASINO YA ODD ONE OUT.

Odd One Out kutoka Meridianbet ni moja ya kasino maridhawa yenye picha halisi, ambayo inakupa nafasi ya kushinda kadri uwezavyo na kuwa milionea mara baada ya mzunguko kukamilika.

CHEZA HAPA

4 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa