“Nimezunguka nchi nyingi za mpira nimetazama Derby nyingi za kidunia, nimeona namna watu wanaandaa mechi zao, nimeona watu wanavyovuna pesa kupitia timu zao kubwa, ila ni tofauti sana kwa Tanzania” Anaandika Shafih Dauda

Niliwahi kusema kitu kuhusu BRAND SOUTH AFRICA, Wizara ya Utalii na Wizara ya Michezo, Chama cha soka Afrika Kusini na klabu za Kaizer Chiefs na Orlando Pirates, wakakubaliana SOWETO DERBY iwe kwenye package hiyo

Soweto Derby
Soweto Derby

Mtalii anaenda Afrika Kusini, lakini ndani yake ana ratiba ya Soweto Derby, ana tiketi ya mechi, anaorder jezi ya timu moja wapo na akiingia uwanjani ananunua vifaa vya moja ya timu, hizo ni hela tupu tunazungumzia, hiyo ni Branding

Branding nzuri imepelekea Makampuni kuweka pesa kwenye derby hii, kila mwanzoni mwa msimu kuna CARLING BLACK LABEL CUP, Hapo inapigwa Derby ya Soweto, hapa kwetu tuliwahi kuwa na Mtani Jembe, ila imekufaje hata sijui

Nini kifanyike kwa DERBY YA KARIAKOO?

Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya michezo na Utamaduni, TFF, TPLB na hizi klabu mbili, wanaweza kutengeneza BRAND TANZANIA, ndani yake iweke KARIAKOO DERBY kama Package, iuzwe kwa Watalii na promo duniani kote

Mtalii anaweza kuja kutalii lakini ratiba yake ikaendana na Dabi ya Kariakoo, hiyo ni pesa kubwa ya kigeni inapatikana, Mtalii ni rahisi kulipa hata dollar 300 kutazama mechi ni kawaida kwa wenzetu, proper branding

 

kariakoo Derby
kariakoo Derby

 

Pia, Dabi yetu haina mvuto uwanjani, hatujui kuwa sio kila anaekuja uwanjani ni shabiki wengine wanapenda kujichanganya, kwanini wasiwepo Wasanii wa kutumbuiza kabla ya Mchezo na Halftime? Kwanini tusiweke burudani kama hizi wakati tunasubiri mchezo? Kuna gharama kubwa?

Kuna ubaya gani ile screen uwanjani ikadisplay mchezo kama wanavyotazama wa nyumbani? Hatuoni kuna utofauti mdogo sana kati ya wa sebuleni na uwanjani? Branding kama hizi ndio huvuta watu uwanjani, lazima tukubali gharama ili kuwa na kitu bora, nje na hapo tutaishi kwa hamasa tu

Lastly, Simba na Yanga wajitambue, Real Madrid na Barcelona inapokuja maslahi na mafanikio wao ni Ndugu, Liverpool na United wanapokuja kwenye maslahi wao ni Ndugu, huku kwetu wanakwama wapi? Wapunguze kujificha ficha, tumieni vyema brand zenu


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu.

Derby, Derby ya Kariakoo Iongezewe Thamani : Dauda, MeridianbetBASHIRI SASA

3 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa