Camp Nou, Barcelona vs Real Madrid. Nalikumbuka lile bao la pili mpaka kesho. Dakika ya 57, pasi ndefu ya Sami Khedira njiani kwa Angel Di Maria. Puyol anamkimbiza, anageuzwa kushoto kisha kulia tena. Puyol anatengua nyonga pale, anawekwa mkao kama anacheza kung fu, mzee na miaka yake 34. Pinto anablock shuti la Angel, ila Ronaldo yupo mtaa, anausukuma kambani. 2-0.

, Di Maria: Sikua na Kipindi kizuri Old Trafford, Meridianbet
Lakini Puyol ajilaumu mwenyewe, lazima itakuwa haongei na wenzake. Angemuuliza ndugu yake Lionel Messi balaa la Di Maria wakiitumikia Argentina pale Beijing kwenye Olympics. Aliwanyoosha Uholanzi kwenye robo fainali kwa pasi yake(Messi). Aliwaburuza Nigeria kwenye fainali, almanusura kipa arudi nyumbani marehemu kwenye fainali.

Angel D maria mbele ya Atletico kwenye ile fainali ya UEFA. Lile bao la pili . Unakumbuka? Aliwaacha mabeki matatu, akampa mateso Courtois kucheza shuti lake, ila Gareth Bale alikuwa mjini, akausukuma tu kwenye wavu. Nalikumbuka tabasamu lake akipewa tuzo ya man of the match na Sir Fergie.

Alipita Benefica kabla ya Madrid. Mtu mmoja pale PSG, Marcin Balla anasema Angel anaichukia man utd haswa. Hata akiona taarifa yao kwenye tv anabadilisha channel. Sijui walimkosea nini ase?

Makala hii imeandaliwa na Deo Mwanasoka.

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa