Baada ya dakika 90 za damu na jasho Camp Nou, Chelsea ya Didier Drogba walirejea darajani wakihitaji ushindi wa aina yoyote ile ili wafanikiwe kutinga fainali ya UEFA 2009.

Bahati mbaya kwao, mechi ya pili muamuzi Tom Hovrebo kutoka Urusi aliwafanyia ‘hujuma ya karne’. Wakiwa mbele bao moja kwa bila, aliwanyima penalti nne za wazi. Chelsea wakaondoshwa nusu fainali ya UEFA kwa bao la dakika ya 93 la Andres Iniesta.

Didier Drogba
Didier Drogba

Baada ya filimbi ya mwisho, Didier Drogba alikuwa na hasira sana. Akamvaa muamuzi na kumshukia kwa maneno makali. Iliwalazimu benchi zima la Chelsea kumshika na kumuondoa Drogba uwanjani.

Wakati Drogba anaondoka uwanjani, alikuja kijana mdogo wa miaka 10 tu akitaka kupiga nae picha. Kwasababu ya hasira Drogba alikataa kupiga nae picha. Akamnyima kutimiza ndoto zake.

Didier Drogba
Didier Drogba

Miaka 10 baadae Drogba alimrudia yule kijana na kupiga nae picha. Safari hii haikuwa uwanjani, bali ilikuwa katika usiku wa tuzo za Ballon d’or. Kijana huyo alikuwa Kylian Mbappe.

UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

kane, Kane Aweka Wazi Maazimio Yake Kucheza UEFA., MeridianbetBASHIRI SASA

3 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa