Borusia Dortmund wanatajwa kuwa wameingia kwenye kinyang’anyiro cha kuiwania saini ya nyota wa Brighton Ben White, wakipata ushindani kutoka vilabu vya Uingereza.

Staa huyu amekuwa kwenye fomu ya kuvutia klabuni hapo kwa msimu huu, akicheza jumla ya mechi 34 za michuano yote.

Mkataba wa sasa wa nyota huyu wa miaka 23 na Brighton unafika tamati Juni 2024. Brighton wanaripotiwa kuwa wanaweza kulazimika kumuuza staa huyu huku Manchester United na Arsenal wakitajwa kuitaka huduma yake Uingereza.

Dortmund, United na Arsenal kwa Ben White

Kwa mujibu wa Mundo Deportivo, Dortmund pia wameungana na vilabu vya EPL kuiwinda huduma ya mlinzi huyu ambaye ana ainishwa kuwa na thamani ya ya euro milioni 35 katika soko la uhamisho la msimu wa joto.

BVB wamesaini hivi karibuni wachezaji wenye moto mkubwa kama Jadon Sancho na Jude Bellingham, na White anaonekana kuwa kwenye kipaumbele cha miamba hawa wa Bundesliga.

Beki huyu wa zamani wa Southampton alianza kufanya vyema katika msimu wake wa mkopo na Leeds United msimu wa 2019-20, kabla ya kuingia kikosi cha kwanza Brighton.


KWANI MERIDIANBET WANASEMAJE! MKWANJA UPO KWENYE KASINO MPYA YA MINI POWER ROULETTE.

Unawezaje kukosa ubingwa ndani ya kasino hii maridhawa, Nafasi ya kushinda mkwanja ni kwa kila mtu, Meridianbet inakupa nafasi ya kuwa mmoja ya washidi leo, unasubiri nini?

Mini Power Roullete

CHEZA HAPA

13 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa