Hakika mwezi Agosti ulikua ni mwezi wenye burudani, visa na mikasa ya kila namna. Mwisho wa siku, viwanja viliamua. Tuzo za EA Sports zatoa washindi wa mwezi.

Mshambuliaji wa West Ham United, Michail Antonio, ametwaa tuzo ya EA Sports Premier League Player of the Month (Mchezaji bora wa mwezi). Antonio alipachika jumla ya magoli 4 na kutoa pasi 3 za magoli katika michezo 3 ya EPL iliyochezwa mwezi Agosti.

Antonio amewashinda Saïd Benrahma (West Ham United), Marcos Alonso (Chelsea), Erick Dier (Tottenham ), Demarai Gray(Everton) na Mason Greenwood (Man United).

EA Sports

Kwa upande wa makocha, Nuno Espirito Santo (Spurs) ameibuka kidedea wa tuzo ya Barclays Manager of the Month (kocha bora wa mwezi) baada ya kuingoza timu hiyo kwenye michezo 3 na kutwaa pointi zote 9 bila kuruhusu goli lolote kuingia kwenye nyavu za timu yake.

Nuno amewazidi kete Rafael Benitez (Everton), David Moyes (West Ham United) na Thomas Tuchel (Chelsea).


USHINDI KIGANJANI KWAKO!

Meridianbet inakuletea ushindi kwenye kiganjani kwako, unafurahia radha halisi ya burudani ya kasino mtandaoni na tabasamu la ushindi.

Meridianbet Online Casino

INGIA MCHEZONI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa