Nchini Uingereza bado hakijaeleweka kuhusu sakata la vilabu 6 vilivyokuwa vimejiunga kwenye mpango wa European Super League. Ed Woodward amechafua hali ya hewa.

Muda mfupi kabla ya United kutangaza kujiondoa kwenye ESL, ilitoka taarifa kuwa Mkurugenzi Mkuu, Ed Woodward ataachia nafasi yake ndani ya klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.

Sababu za Woodward kuondoka United bado hazijawekwa wazi na hivyo kuacha hali ya sintofahamu kwamba ni kwanini aondoke sasa hivi? Kuna nini kimemuondoa United? Kila mtu amebaki na majibu yake na pengine ukweli anaujua Woodward mwenyewe.

Hali ni tofauti miongoni mwa viongozi wa serikali nchini Uingereza. Imeripotiwa kuwa, siku 4 kabla ya kutangazwa kwa ESL, Woodward alihudhuria kikao na viongozi wa serikali kule Downing Street.

Kikao hiki kiliongozwa na afisa kutoka ofisi ya Waziri Mkuu, Boris Johnson (Dan Rosenfield). Gazeti la The Sunday Times la nchini Uingereza, liliripoti kuwa miongoni mwa vilivyojadiliwa, ilikuwa ni European Super League.

Ed Woodward, Ed Woodward Achafua Hali ya Hewa Uingereza., Meridianbet
Dan Rosenfield

Hii ni taarifa tofauti na iliyotolewa na msemaji wa waziri mkuu, kwa mujibu wa msemaji huyo amesema, kikao cha Rosenfield na Woodward, hakikujadili ESL. Wakati wa kikao hicho, Woodward alipata pia wasaa wa kutambulishwa kwa ufupi kwa Boris Johnson.

Akijibu kuhusu utambulisho wa Ed Woodward kwa Waziri Mkuu, Boris Johnson, msemaji wa Johnson amesema “Kulikuwa na utambulisho mfupi sana kwa Woodward. Nadhani waliwahi kukutana. Lakini European Super League haikujadiliwa.

Baada ya kuulizwa zaidi pengine Dan Rosenfield alimuahidi Woodward kuwa mpango wa European Super League hautopingwa na serikali, msemaji wa Waziri Mkuu amesema “Hapana, hiyo sio sawa. Majadiliano yalikuwa kuhusu usalama wa kuwarudisha mashabiki sambamba na vyeti vya Covid kama sehemu ya mpango wa kurejea kwa michezo.”

Bado kuna hali ya sintofahamu miongoni mwa wanasiasa nchini Uingereza kuhusu mkutano wa Ed Woodward na viongozi wa serikali. Vyama mbalimbali vimezungumzia kikao hiki ambacho kimepewa jina la Namba 10.

Ed Woodward, Ed Woodward Achafua Hali ya Hewa Uingereza., Meridianbet
Vilabu 6 vya EPL vilivyokuwepo kwenye mpango wa European Super League.

Kabla ya ripoti ya kikao Namba 10, Jo Stevens kutoka chama cha Labour alisema “Johnson anapaswa kuuambia umma ni kitu gani kilizungumzwa wakati Woodward alipowatembelea.”

Katibu kivuli wa Utamaduni alisema ” Umma unahaki ya kuambiwa ni kitu gani serikali iliwaahidi Manchester United kupitia viongozi wote na Waziri Mkuu. Kama Boris alisapoti European Super League na kisha kuwakana hadharani, waingereza wanastahili kuambiwa ukweli wote na kuombwa msamaha haraka sana.”

Kwani Ed Woodward na Boris Johnson wao wanasemaje katika hili? Hakika sakata la European Super League limezua mjadala mzito!


KWANI MERIDIANBET WANASEMAJE! MKWANJA UPO KWENYE KASINO MPYA YA MINI POWER ROULETTE.

Unawezaje kukosa ubingwa ndani ya kasino hii maridhawa, Nafasi ya kushinda mkwanja ni kwa kila mtu, Meridianbet inakupa nafasi ya kuwa mmoja ya washidi leo, unasubiri nini?

Mini Power Roullete

CHEZA HAPA

12 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa