Kipa namba moja wa Manchester City Ederson amefanikiwa kuchukua tuzo ya kipa bora wa msimu kwa mara ya pili mfulululizo akiwa amecheza mechi 190 toka ajiunge na mabingwa hao wa EPL mwaka 2017, Kipa huyu anakuwa ni kipa wa pili wa Man City kufanya hivyo toka Joe Hart afanye hivyo mwaka 2010 mpaka 2013.

Ederson1
Ederson akiwa na Guardiola baada ya kuchukua tuzo ya kipa bora 2020

Mchezaji huyu mwenye umri wa miaka 27 amechukua gloves hizo za dhahabu akiwa na clean sheets 18 na kumshinda mpinzani wake, Edouard Mendy ambaye alifungwa goli na Iheaanacho, na kwa sasa hata kama Mendy hatofungwa mechi ya mwisho atakuwa na Clean sheets 17 tu tofauti na hizi 18 za kipa wa City.

Ukuta wa Manchester City umekuwa sehemu muhimu sana ya kuwasaidia City kuchukua ubingwa wa EPL msimu huu na Ederson akiwa na Clean sheets 18 inaonesha namna ambavyo ana umuhimu klabuni hapo.

Mchezaji huyu wa kibrazil amefanikiwa kutoruhusu kufungwa katika mechi 18, huku akioka mipira 63, na kugusa mpira mara 1198 na kutoa pasi zaidi ya 900. Ederson atapewa tuzo yake hii katika mchezo wao wa mwisho dhidi ya Everton wikiendi hii.

UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

ederson, Ederson Achukua Kipa Bora Kwa Mara Ya 2, MeridianbetBASHIRI SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa