Kunako muendelezo wa EPL, Man United wanakibarua cha ziada kuelekea mwishoni mwa msimu wa 2020/21. Siku 8 za maangamizi kwa vijana wa Ole Gunnar Solksjaer.

Baada ya mchezo wa United vs Liverpool kughairishwa jumapili iliyopita, mchezo huo umeongeza idadi ya mechi za EPL zilizosalia kwa United kukamilisha msimu huu.

Badala ya kuwa na michezo 4, United watakuwa na jumla ya michezo 5 ya Ligi Kuu iliyosalia kwenye kalenda ya 2020/21.

Idadi ya michezo 5, inapelekea Man United kuwa na jumla ya michezo 3 ambayo itachezwa ndani ya siku 8. Tarehe 9, Mei – Man United watawafata Aston Villa kule Villa Park kabla ya kuwakaribisha Leicester City pale Old Trafford tarehe 11, Mei.

Baada ya Leicester City, itakuwa ni zamu ya Liverpool kuingia Old Trafford kumenyana na United (Mei 13, 2021). United watapumzika kwa siku 4 kabla ya kuwaalika Fulham katika mchezo wa mwisho wa EPL kuchezwa kwenye uwanja wa Old Trafford kwa msimu huu.

Man United watamaliza msimu kwa kuwafuata Wolverhampton, Mei 23, 2021. Endapo Man United watafuzu hatua ya fainali ya Europa, basi watacheza mchezo wa fainali Mei 26, 2021. Hakika huu ni mwezi wa maangamizi kwa United.


TENGENEZA FAIDA KUPITIA MCHEZO WA TITAN DICE UKIWA NA MERIDIANBET KASINO

Unapokuwa kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, huna sababu ya kucheza kwa mashaka. Titan Dice, ni mchezo unaweza kukupatia mamilioni kwa mzunguko mmoja!

EPL, EPL: Siku 8 Za Maangamizi Man United, Meridianbet

SOMA ZAIDI

15 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa