Erling Haaland huenda akatua katika dimba la Camp Nou baada ya wawakilishi wake kuanza mazungumzo na klabu ya Barcelona.

Siku ya Alhamisi asubuhi baba wa straika huyo ambaye pia ni mshauri wake Alf-Inge Haaland na wakala Mino Raiola walionekana katika uwanja wa ndege wa Barcelona.

Kulingana na vyanzo vya habari vya michezo wa nchini Spain wawili hao walionekana wakiendeshwa kwenye gari na rais wa klabu ya Barcelona Joan Laprta.

Rais huyo mpya alimuorodhesha starika huyo wa Borussia Dortmund wakati wa kampeni kabla ya kushinda kiti cha urais mwezi uliyopita.

Klabu inapitia kipindi kigumu kiuchumi wakati pia inajaribu kurekebisha mkataba wa mshambuliaji Lionel Messi ambao unatarajiwa kuisha mwezi Juni.

Lakini taarifa zinadai Raiola na Laporta wamekuwa na uhusiano imara wa kufanya kazi pamoja, hivyo basi kuna uwezekano mkubwa wa Barca kushinda mbio za kumnasa Haaland.

SunSport ilisema wiki hii kwamba dili ya mchezaji huyo wa miaka 20 inaweza kugharimu kiasi cha £300m

Hiyo itajumuisha £150m ada ya uhamisho na mkataba huo wa miaka mitano utahusisha £600,000 kama mshahara wa mchezaji huyo kwa wiki.


UNAWEZAJE KUKOSA KASINO YA BREAK AWAY LUCKY WILDS INAYOKUPA NAFASI YA USHINDI MURUA.

Break Away Lucky Wilds ni moja ya Sloti pendwa katika kasino za #meridianbet inayokupa mara 11,000X ya dau lako, unayo nafasi ya kuwa milionea unasubiri nini?

CHEZA HAPA

7 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa