Kandanda safi inaendelea kupepetwa katika nchi ya Ufaransa na kwenye mechi ya pili ya Kundi C la EURO 2016 iliyochezwa usiku wa Jumapili huko Stade Pierre Mauroy mjini Lille, mabingwa wa dunia Ujerumani waliibuka kidedea kwa ushindi wa bao 1-0.

Ujerumani walifunga bao lao dakika ya 19 kwa kichwa cha Mustafi aliyeunganisha fri-kiki ya Toni Kroos toka kwa winga ya kulia ambapo hadi mapumziko Ujerumani 1 na Ukraine 0. Mnamo dakika ya 89, Ujerumani walimuingiza nahodha wao mkongwe Bastian Schweinsteiger ambaye sasa yupo na Manchester United na ambaye amekuwa nje ya uwanja tangu Machi 20 akiuguza goti na dakika 1 baadaye akaipa Ujerumani bao la pili baada ya kaunta-ataki safi iliyoishia kwa krosi safi ya Mesut Ozil.

Mchezo uliongozwa na refarii wa Uingereza bwana Martin Atkinson. Awali jana, katika mechi nyingine ya Kundi C, Poland waliichapa Ireland ya Kusini 1-0. Leo mabingwa watetezi Spain kuanza na Jamhuri ya Czech!

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa