Belgium Yashinda 2-0, Lukaku Aendeleza Rekodi!

Michuano ya Euro 2020 iliendelea hapo jana ambapo timu ya kwanza kwa ranki ya FIFA duniani, Belgium ilifanikiwa kutinga hatua ya 16 bora baada ya kuwachapa Finland bao 2-0 na kufikisha alama 9.

Katika mechi hiyo, Belgium walikuwa kwenye moto sana na walishambulia lango la Finland kwa mara nyingi sana, huku wakipiga mashuti 17 na kati yao ni saba tu ndio yaliylenga lango la Finland.

Ushindi wa Belgium unakuwa ni wa 3 katika hatua ya makundi yaani wakiwa wameshinda michezo yote mitatu ya hatua ya makundi kama walivyofanya katika hatua ya kufuzu kushiriki michuano hiyo ambapo walishinda michezo 10 kati ya 10.

Shujaa wa mchezo huo alikuwa ni yule yule Kevin De Bruyne akisaidiana na Romelo Lukaku ambaye bado anaendelea kuonesha ubora wake katika michuano hiyo kwa kufunga goli la tatu la hatua ya makundi.

Belgium

Lukaku na De Bruyne wameonekana kuwa muhimili muhimu sana kwa Belgium ambao wanaonekana wapo kwenye moto na wanaweza kubeba kombe hilo endapo tu wataendeleza makali hayo hayo wanayoonesha sasa!


USHINDI BILA MIPAKA!

Hakuna mipaka ya ushindi kwenye Keno Instant ya meridianbet Kasino, hii wewe ndiyo una uamuzi zaidi juu ya mchezo na nafasi ya machaguo kibao.
Arsenal, Arsenal Wawasilisha Ofa ya Pili Joaquin Correa., Meridianbet

Acha ujumbe